Katibu
Tawala Wilaya Sengerema Bw. Focus Majumbi, (katikati) akishudia nyavu
haramu kabla ya kuchomwa. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu msngi Wilaya
Sengema Juma Mwajombe na Kulia ni Afisa uvuvi shupavu Bw. Henry
Kaswahili.
Na Daniel Makaka wa MOblog, Sengerema
Zana
haramu za kuvulia Samaki zinazokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi
milioni mia mbili na laki tani zimekamatwa na kuteketezwa na Afisa uvuvi
tarafa ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Bw.Henry Kaswahili.
Kwa
mujibu wa taarifa yake katika hafla ya kisomo cha watu wazima, ambayo
pia ilitumika kuchoma zana hizo haramu, zana zilizochomwa ni pamoja na
Kokolo 8 za Sangara; Timba 2,525; Kokolo za dagaa 3; Mitubwi 33
iliyokuwa inajihusisha na uvuvi haramu na nyavu ndogondogo 50.
Kwa
ujasiri huo, Katibu tawala wa wilaya Sengerema Bw. Focus Majumbi
amempongeza Afisa huyo na kusema ni mfano wa kuigwa kwa kukamata nyavu
haramu na kuziteketeza kwa moto.
Afisa uvuvi Henry Kaswahili akianda nyavu haramu ili zichomwe moto.
Akiwa
mgeni rasmi katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima Wilayani
Sengerema yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakalilo Tarafani Buchosa
ambako kazi ya uchomaji wa nyavu hizo haramu ilifanyika alisema kiongozi
huyu anapaswa kupongezwa kutokana na umahili wake wa kukamata zana hizo
kisha kuziteketeza kwa moto.
Kwa
upande wake Afisa uvuvi huyo alisema ameamua kupambana na uvuvi huo
haramu kwakuwa umekithiri na umekuwa tishio wilayani Sengerema na
ameahidi kuutokomeza katika maeneo anayoyaongoza akishirikiana na na
raia wema.
Nao
wananchi waliokuwa wamekusanyika kushuhudia uchomaji wa nyavu hizo
haramu pamoja na viongozi wengine wamempatia sifa lukuki kwa kuonesha
nia na njia ya kudhibiti uvuvi haramu wilayani humo.
Viongozi na wananchi wakishudia zoezi la uchomaji nyavu haramu.
Wananchi wakishudia na nyavu haramu kuteketezwa.