WAUMINI WA KANISA LA ANGLIKANA NYAMAGANA WALETA VURUGU KANISANI, WAMTUHUMU ASKOFU WAO KUWA NI FREEMASONS


 


Waumini wa kanisa la Anglikana Wilaya ya Nyamagana Mwanza walisimamisha kwa muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea vurugu kubwa.

 Vurugu hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu wa kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa 
tamko la jinsi askofu wao anavyofanya kazi na kundi la Freemason ndipo waumini walipomvamia na kumtoa nje ya kanisa kwa nguvu na kusababisha vurugu kubwa.

Muumini huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa askofu huyo pia hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo kutaka kubomoa sakafu akidai kuna irizi imefichwa na baadhi ya  waumini wake kanisani hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo