Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma |
Watu
saba wameuwawa vibaya kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali
kwa kuhusishwa na imani za kishirikina,huku nyumba ishirini zikichomwa
moto katika kijiji cha Murufyiti,wiliaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani kKasulu mkoani Kigoma |
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,Japhari
Muhamed amesema,tukio hilo lilifanyika juzi majira ya saa nne usiku
baada ya M/kiti wa kijiji hicho aitwaye Evarist Ruhaya akishirikiana na
mganga wa jadi,Faustino Ruchagula kupiga mbiu ya hatari ili kukusanya
watu na kufanya unyama huo.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma |
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani kKasulu mkoani Kigoma |
....amesema
watu waliouwawa ni ,John Muvuma (68),Elizabeth Kaje (55),Dyaba Kitwe
(55),Vincent Ntiyaba (42),Helman Ntabiloye (78),Redamta Mdogo (60) na
Ramadhani Kalaliza (70) wote wakiwa ni wakazi wa kjiji hicho cha
Murufyiti,pia nyumba18 zilichomwa moto na zingine mbili kubomolewa na
kutimiza idadi ya nyumba20
....kamanda
Mohamed amesema,tayari watu13 akiwemo mwenyekiti wa kijiji wamekamatwa
kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kuhakikisha wote
waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma |
.....nae
mtendaji wa kijiji hicho Ogeni Gaspa amesema kabla ya wauaji kuanza
alipiga simu kwa OCD ili polisi waje kutuliza ghasia lakini gari
hazikuwepo kituoni hivyo hali iliyopelekea Polisi kufika eneo la tukio
kwa kuchelewa na kukuta mtu wa mwisho akiuwawa.
....kwa upande wa mtoto mmoja wa marehemu,aliejitambulisha kwa jina
la Josiphat John amesema:-wakati tukio hilo linaendelea kwa wazazi wangu
nilishindwa kutoka nyumbanikwangu kwa hofu ya kudhulika lakini
ilipofika alfajiri nilikwenda kuangalia miili ya wazazi wangu ndipo
nilipokuta imeteketezwa na moto...
Mwisho wa Habari.
Makaburi haya mawili niya watu waliouwawa kwa kuchomwa moto katika tukio hili na kuzikwa hapa.PICHA NA HOTNEWS KASULU. |