WAKAZI
wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani
Mtwara wamefikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani kujibu shitaka
linalowakabili la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya vigodoro kwenye
sherehe ya ndoa.
Jemima
Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) pamoja na mtoto
mwenye umri wa miaka 17 (Jina linahifadhiwa) walifikishwa mahakamani
hapo juzi mbele ya Hakimu Halfani Ulaya na kusomewa shitaka na mwendesha
mashtaka Iddi Athumani.
Athumani
alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu
majira ya saa 12 jioni katika eneo la Masasi Mbovu huku wakijua kuwa
kufanya hivyo ni kosa linalokwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Alidai
kwa kuwa shauri hilo linamshirikisha mtoto aliye chini ya miaka 18, ni
vyema Mahakama ikaahirisha kesi hiyo ili kupisha upelelezi wa kina
kuhusu shitaka hilo linalowakabili washtakiwa hao.
Hakimu
Ulaya alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka na aliahirisha kesi
hiyo hadi Oktoba 30 mwaka huu itakapotajwa tena. Watuhumiwa hao walio
nje kwa dhamana hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo.