WANAFUNZI WACHOMA MOTO SHULE YA SEKONDARI NJOMBE, SERIKALI YAIFUNGA KWA MUDA WA MWEZI MMOJA


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe, Fulgence Ngonyani akiangalia bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe ambalo limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Jana.

Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe (Njosi) wakati wakisubiri kupelekwa kituo cha polisi.

Askari akimwangalia mmoja wa wanafunzi ambaye anapelekwa kupakizwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Na Michael Ngilangwa NJOMBE

Kamishna wa Elimu Nchini Ameifunga Shule ya Sekondari ya Njombe (NJOSS) Kwa Muda wa Mwezi Mmoja Kutokana na Vurugu Zilizotokea Katika Shule Hiyo na Kusababisha Hasara ya Zaidi ya Shilingi Milioni Moja.

Akifunga Shule Hiyo Kwa niaba ya Kamishna wa Elimu Nchini, Afisa Elimu Shule za Sekondari Mkoani Njombe Said Nyasiro Amesema Wameifunga Shule Hiyo Kutokana Uharibifu Uliofanywa na Wanafunzi Ikiwemo Kuchoma Jengo la Bweni na Karakana Pamoja Kupisha Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo.

Aidha Afisa Elimu Huyo Ameongeza Kuwa Kila Mwanafunzi Atatakiwa Kurejea Shuleni Hapo Akiwa na Mzazi Ama Mlezi Wake Pamoja na Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini Kwa Ajili ya Kufidia Mali Zilizoharibiwa .

Akizungumzia Chanzo cha Tukio Hilo Mkuu wa Shule ya NJOSS  Benard William Amesema Huenda Likahusishwa na Maamuzi ya Bodi ya Shule Hiyo Iliyokutana  Oktoba 7 Mwaka Huu na Kuwasimamisha Masomo Wanafunzi Waliotoroka Nyakati za Usiku na Kwenda Kwenye Disko Katika Chuo cha Maendeleo Mjini  NJombe, Huku Akisema Kuwa Uchunguzi Bado Unaendelea Kuhusiana na Tukio Hilo.

Hata Hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Linawashikilia Kwa Mahojiano ya Kina Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Njombe NJOSS  Wanaosadikiwa Kuhusika Katika Tukio Hilo.

Mwanzoni Mwa Mwaka Huu Kulitokea Ajali ya Moto Katika Shule ya Sekondari Njombe na Kusababisha Uharibifu wa Baadhi ya Majengo Wakati Wanafunzi Wakiwa Katika Masomo ya Usiku PrepO.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo