WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA UGALI WA MUHOGO WENYE SUMU HUKO MULEBA

Watu wawili wamefariki dunia Wilayani Muleba baada ya kula ugali wa muhogo unaosadikiwa kuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Mwaibabe alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo mama na mtoto wake walifariki dunia huku ndugu wengine wanne wakiendelea kutibiwa hospitali.

Alisema familia hiyo ilinunua udaga kwa ajili ya kusaga unga na baada ya kuutumia hali zao zilibadilika na kukimbizwa hospitalini ambapo mama na mwanaye wa miaka mitano walifariki njiani kabla ya kufikishwa hospitali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo