Naibu
Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Wapili
kushoto) akizungumza na Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya
China wakati walipofanya ziara nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji
(Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe.
Naibu
Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw.
Paul Sangawe akizungumza wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Na Saidi Mkabakuli
Ugeni
kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China imevutiwa na kasi ya
ukuaji wa uchumi wa Tanzania hali inayochochewa na mipango thabiti ya
kuvutia uwekezaji hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs).
Akizungumza
wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania,
Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa
nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya kufikia maendeleo na
kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya kipindi kifupi
kijacho.
Bw.
Jianjun aliongeza “ili kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi,
Tanzania inapaswa kuwekeza katika viwanda ili kuongeza tija katika
uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje
ya nchi.”
Akizungumza
wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Naibu Katibu Mtendaji
anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw.
Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuwa nchi ya viwanda
ndani ya muda mfupi ujao.
“Tumedhamiria
kuwekeza nguvu zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa
Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili
kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw.
Sangawe.
Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi
yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka
2025.