Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia January Makamba (Kulia) akizungumza
katika mkutano wa wadau wa teknolojia ya Tehama (Capacity Africa 2014) ambapo
amesema serikali itaondoa tatizo la mawasiliano nchini na huku ikitarajia
kusambaza huduma hiyo kwa vijiji 1,800
ifikapo mwakani na vijiji 4,000 ikikapo mwaka 2017. Kushoto kwa Naibu Waziri
Makamba ni mkurugenzi wa kampuni ya
Seacom Byron Clatterbuck na Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh
Padayachee.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Six Telecoms,
Rashid Shamte akifafanua jambo kuhusiana na maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini.
Kampuni hiyo ni moja ya wadhamini wa mkutano huo unaofanyika nchini kwa mara ya
pili. Kulia ni Ofisa Biashara mkuu wa
kampuni hiyo, Tinashe Bgoya.
Ofisa
Biashara mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Tinashe Bgoya (kushoto) akizungumzia
maendeleo ya maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini. Kulia ni Saidi Mohmed
Alli ambaye ni Mkuu wa kitengo cha ‘Data’ cha kampuni hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (Kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano ya Tehama ujulikanao kwa jina la Capacity Africa. kampuni hiyo ni moja wa wadhamini wa mkutano huo. Kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh
Padayachee.
======== ===== ===== =======
Dar es Salaam. Jumla ya vijini 1,800
vinatarajia kupatiwa mawasiliano ya simu ya na teknolojia ya mawasiliano ya
habari na mawasiliano (Tehama ) ifikapo mwakani.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa
wadau wa Tehama wa Africa (Capacity Africa), Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema kuwa mpango huo upo katika hatua
za mwisho na ifikapo mwaka 2017, jumla ya vijiji 4,000 zitakuwa vimepatiwa
huduma hiyo.
Makama alisema kuwa serikali ipo katika
hatua za mwisho kuzungumza na kampuni ya
simu kutoka Vietnam ijulikanayo kwa jina la Viettel na hivi karibuni
wanatarajia kuzindua rasmi mpango huo.Alisema kuwa kuna vijiji mbali mbali Tanzania
havina kabisa mawasiliano na jukumu la serikali kuhakikisha kuwa tatizo hilo
linatatuliwa.
Kwa mujibu wa Makamba sekta ya mawasiliano
inazidi kukuwa na serikali imeweka mpango maalum kuhakikisha kila Mtanzania
anapata huduma hiyo tena kwa ubora wa hali ya juu. Alisema kuwa sekta hiyo ina changamoto
nyingi kutokana na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano na tayari serikali
imechukua hatua kukabiliana na tatizo hilo hasa baada ya kukamilika kwa hatua
ya tatu ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano.
“Mpaka sasa ni mkoa wa Simiyu tu
haujafikiwa na mkongo wa taifa na hiyo imetokana na kugawanywa kwa mkoa wa
Shinyanga, hata hivyo mikakati inafanyika ili kuhakikisha mkoa huo unapata
huduma hiyo na kuanza kufurahia huduma ya Tehama,” alisema Makamba.Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms,
Rashid Shamte alisema kuwa anaamini kuwa kukamilika kwa mkongo wa Taifa
kutanufaisisha nchi jirani ambazo hazina bahari.
Shamte ambaye kampuni yake ilidhamini
mkutano wa mwaka 2012 alisema kuwa wanafuraha kubwa kuona nchi inafanya juhudi
za kutatua tatizo la mawasiliano vijijini na nchi takribani nane zinazoizunguka
Tanzania.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alisema kampuni yao imeanzisha kitengo cha
mtandao wa internet ambacho kitatoa huduma hiyo kwa bei nafuu.
“Lengo letu kubwa ni kurahisisha
mawasiliano, hivyo tunawahikikishia kuwa watu wote wanaoishi vijijini watapata
huduma hii kwa bei nafuu,” alisema
Ngota.