Mkazi wa Kijiji cha Ilogi Kata ya Bugarama wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga Simon Waganda (58-60) amekufa
papo hapo baada ya kukatwa na jembe kichwani na Mtoto wake Matokeo Simon
(22) Baada ya kutokea ugomvi wa shamba.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha IlogIi Stephano Matinde amesema
Tukio hilo lilitokea oktoba 13 majira ya saa mbili asubuhi wakati Matokeo Simoni
akifanya maandalizi ya shamba kwa lengo la kujiandaa na msimu wa Masika.
Shamba hilo hilo linadaiwa lilikuwa la baba yake Mzazi ambapo Simon
Waganda ambaye ni Marehemu alifika Shambani hapo na kuanza kumuuliza kwanini
anaandaa shamba ambalo baba si mali yake kwani tayari alikuwa amewagawia ndipo
ugomvi ulipoanza.
Matinde amesema Baada ya ugomvi ndipo kijana huyo alipomkata baba yake na Jembe sehemu ya Kichwani na kufa papo hapo
kutokana na kuvuja damu nyingi na kwamba kijana huyo inasadikika kuwa ana upunguifu wa akili.
Amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo uongozi wa Kijiji ulipewa
taarifa na baadhi ya mashuhuda ambapo nao waliamua kulijulisha jeshi la Polisi
Wilayani humo ambalo lilifika na kumkatamata mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano
zaidi.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa Wa Shinyanga
Justus Kamgisha amesema kwa sasa jeshi la Polisi linamshikilia kijana huyo kwa
upelelezi zaidi na upelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa
mahijiano zaidi.