NA KENNETH
NGELESI,EDDY BLOG MBARALI
VIJANA
katika kata ya Igurusi wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wameaswa kujenga
utamaduni kuwa na ujasiri wa kuthubutu
katika masuala ya maendeleo na yenye tija
badala, ya kuwa tabia hiyo katika maovu ambayo yatapelekea kupoteza mwelekeo
wa maisha.
Rai hiyo
ilitolewa hivi karibuni na Ofisa Maendeleo, kata ya Igurusi, Zainabu Kinyaga katika
Viwanja vya shule ya Msingi Majenje katika kata hiyo,wakati wa uzinduzi wa
kampeni za upimaji wa hiari wa VVU na UKIMWI kwa wakazi na kata hiyo
unaoratibiwa na mtandao wa wakulima nchini (MVIWATA).
Alisema kuwa
asili, vijana ni watu wenye nguvu ambao
siku zote ni watu wa kuthubutu lakini wengi wao wamekuwa wakitumia uthubutu huo katika mambo mabaya yakiwemo masuala ya
ngono zembe ambayo hupelekea wengi wao kupata maambukizi ya vvu.
Akizumunguza
na eddy blog hivi karibuni, mara baada ya zoezi la ufunguzi wa Kampeni ya
upimaji wa VVU na UKIMWI,ambayo inafanyika katika Shule ya Msingi Majenje,Kinyaga
alisema ni vema vijana wakabadilika na kuwa watu wa kuthubutu katika masuala
yenye tija na mendeleo kwa mustakabali wa taifa.
‘Niwaombe
vijana wawe na ujasiri wa kuthubutu kama ilivyo kawaida yao, kwani walio wengi ni wepesi wa kuthubutu lakini
ni vema uthubutu wao ukawa katika vitu vya msingi na vyenye tija kwa jamii
inayo wazunguka na taifa kwa ujumla’ alisema Kinyaga
Aidha katika
hatua nyingine Ofisi huyo aliwataka vijana kutambua mchango Mkubwa ulifanywa na
MVIWATA wa kuwaletea huduma ya upimaji wa afya zao, na kwamba ni vizuri kupima ili waweze kujitamabua.
Alisema kuwa
mtu yeyote anayeijua afya yake ni rahisi kufanya mipango yake, pia itakuwa rahisi
kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Awali
akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi mratibu wa Kampeni hizo Hasira Zahoro aliwataka
wananchi kutoka vijiji nane vya kata ya Igurusi kutambua wazi kuwa maambukizi
katika kata hiyo yapo na hasa kutokana mungiliao wa watu katika soko la Mchele
Igurusi na barabara kuu ya Tanzania
Zambia ambapo kata hiyo imekuwa ikitumika kama maegesho ya magari.
Zahoro
aliongeza kuwa kampeni hiyo iliyonza Oktoba 23 mwaka huu kilele chake ni Oktoba
28 na kwamba lengo ni kupima watu zaidi ya 500 kutoka kata hiyo yenye vijiji vya
Rwanyo, Ilolo, Majenje, Igurusi, Lunwa, Chamoto, na Uhambule
Zahoro
alisema kuwa mbali na kutoa huduma ya kupima lakini pia wanatoa ushauri
mbalimbali kwa vijana ikiwemo kujishuhulisha na masuala ya kilimo ambapo kwa
asilimia kubwa yanakimbiwa na kundi kubwa na vijana.
Aidha katika
hatua nyingie Mratibu huyo alisema kuwa kampeni hizo zimelenga wadau wote wa
Soko hilo ambao ni, wakulima,wabeba mizigo,Wamiliki wa
mashine za kukoboa Mpunga,na wafanyabishara wanao fika kununua bidhaa katika
soko hilo.
Hata hivyo
ili kuongeza hamasa kwa vijana kushiriki vyema zoezi la upimaji pamoja na
kupata elimu katika masuala ya kilimo
Mviwata iliamua kuendesha mashindano ya soka kwa vijana kutoka vijiji
nane ambapo bingwa atapatikana siku ya kilele cha upimaji Oktoba 28 mwaka huu
katika uwanja wa shule msingi Majenje.