Watu wawili ambao
hawajafahamika wamefariki dunia papohapo, leo mchana baada ya gari ndogo
aina ya Carina waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la
kampuni ya Happy Nation wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika kijini cha Chekereni katika mji wa Hedaru Wilayani humo huku pia abiria wapatao wanne waliokuwepo katika basi hilo wakipata majeraha katika maeneo mbalimbali ya miili yao.

Kwa mujibu wa mashuhuda
wa ajali hiyo, gari hiyo ndogo yenye namba T 653 BZR iliyokuwa ikielekea
mkoani Kilimanjaro ilitoka na kuingia upande wa kulia na ndipo
ilipogongana na basi hilo lenye namba T 702 BUW lilikuwa likitokea
mkoani Arusha.
Jeshi
la Polisi Kitengo cha usalama Barabarani limefika eneo la tukio na
kufanikiwa kutenganisha magari hayo, wakichukua kuku wakichukua viungo
vya miili ya marehemu hao ambao hawatambuliki kutokana na kusagika
vibaya.