UPDATES; PICHA ZA MAITI ZILIZOOPOLEWA HADI SASA KUFUATIA AJALI YA MITUMBWI ZIWA TANGANYIKA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-vGpwtFN-mSWiWFYD7KdAFTW1hupaWtWn6utDWxwqdVreEQYbi8SsktoC9G1P3we7xsJkftS1mFLdUIgMQ-EsGqWequTV09wG6N9MUzj_-CaoDS_df433-CRitmKBr_oSDfyW2THx2608/s1600/unnamed+(35).jpgWanajeshi wa Jeshi la Wananch (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama

Na Editha Karlo wa Globu ya jamii Kigoma 

Mpaka sasa jumla ya maiti nne zimeopolewa na kufanya kufikia idadi ya maiti kumi zimepatikana katika ajali ya mitumbwi iliyotokea jana mchana katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi iliyokuwa imebeba maharusi ndugu jamaa na wapambe kupigwa wimbi na kuzama. 

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya Mkoa amesema kuwa bado idadi maiti zilipo kwenye maji ni kubwa ambazo bado hazijapatikana. 

 ''Zoezi hili linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu duni ambavyo ni kikwazo katika zoezi hili la ukoaji. Lakini bado tunaendelea na kazi ''Mkuu wa Mkoa huyo ameiambia Globu ya Jamii asubuhi hii.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvgNa1DGTHNHZXg_xlGdySqSX2MnHE1i0yVgSfUnZ7rA0ZURQ-Zsq8sQPrGk38nymrfBm1DbOd78BhtXMrtBxOTFa_ZXsIJ60OauUmjregQCyoqkVcZ03FoYJKX36gGUXHsvz5ra19yWMy/s1600/unnamed+(36).jpgZoezi la uopoaji wa miili linaendelea na vikosi mbalimbali vya ukoaji katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdHLdVjDpU3U9NBQDB8cm7qrvhk3ONhHl2xYko2z5H1t6g_7ePk7H4znrO3GvHjnZL733qSXS6-0F0p4nhKfCKGz7NEWrD1fHXHhGUM36t94_tQiWAgvVHCie1fclAHBnwnLJ-dEolb5yd/s1600/unnamed+(34).jpgWaokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana katika ziwa Tanganyika baada ya ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4jGSBi1W_8hbbvAA46e5orWLGBQFC82l3uhdYB8cVcb4DcqUHLgIOCeTzQC5m744gp0_kCi43VTK1WRQXD9DeuquKF-T5KJIf6Gtk-cclZAmXOO07TDL7MA23QOnrbUraAw6OMsdoiZNT/s1600/unnamed+(33).jpg Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana. Nao ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya (wa pili kushoto) anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Kigoma


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo