UNAIKUMBUKA ILE KESI YA JAMAA KULAWITIWA BAADA YA KUNASWA NA MKE WA MTU, SHAHIDI AFUNGUKA MAZITO MAHAKAMANI

Shahidi wa kwanza katika kesi ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii inayowakabili wakazi wawili wa Mbagala, ameieleza Mahakama kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mlalamikaji kwa kipindi cha miaka saba, huku akiwa na mume wake ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo.
 
Shahidi huyo, Sanifa Sadick alidai mahakamani hapo jana wakati akitoa ushahidi kuwa mshtakiwa, Erick Kasira (39) ni mume wake tangu mwaka 2006 na wana watoto wawili.

Sanifa alisema kuwa Agosti 23 mwaka huu, waliwasiliana na mlalamikaji ili wakutane nyumba ya kulala wageni ya Maembe Bar & Guest House iliyopo, Yombo Kiwalani kwani alikuwa na shida ya Sh100,000.

Shahidi huyo alidai kuwa wakati anaelekea eneo la tukio kwa usafiri wa bodaboda, aliona pikipiki nyingine ikifuatilia kwa nyuma hadi eneo hilo.

“Nilikuwa na shaka wakati pikipiki nyingine ikitufuatilia kwa nyuma,” alisema shahidi huyo katika utetezi wake.

Alidai kuwa alimkuta mlalamikaji peke yake na kuagiza kinywaji, kabla ya kuchukua chumba namba sita na wakiwa ndani, mlango wa chumba uligongwa na ndipo alimuona mume wake akiwa na vijana watatu ambao hakuwafahamu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kufanya vitendo vya ulawiti kwa mlalamikaji baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Sh1 milioni kama adhabu ya kukutwa na mke wa mtu.

 Washtakiwa hao wanadaiwa kumlawiti Idd Kambi baada ya kushindwa kutoa Sh 1milioni kwa madai kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mmoja wa washtakiwa hao.

Washtakiwa walimkuta mlalamikaji Kambi akiwa na Sanifa Bakari katika chumba namba sita na hivyo kumshtumu kuwa ana mahusiano ya kimapezi na mwanamke huyo kutokana na mshtakiwa mmoja kudai kuwa ni mke wake na kwamba wamemfumania

Hata hivyo hakimu Mfawidhi wa Mahakam mahakama hiyo, Said Mkasiwa aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 3 mwaka huu itakapoendelea.

Na Hadija Jumanne


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo