Zimezagaa taarifa kuwa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya (PICHANI juu), amerushiana risasi za moto na mwanaye wa kumzaa, Jonas Nkya ndani ya ofisi zao mkoani Morogoro muda huu.
Lakini Kwa mujibu wa mtoto wa waziri huyo John Nkya (pichani chini) ambaye amezungumza na mwandishi wa habari Hilda Mushi amekana kurushiana risasi na mama yake mzazi na kusema hakuna kitu kama hicho
Amesema ukweli ni kwamba alikuwa amekwenda kwenye eneo la ofisi yao kwa ajili ya kwenda kuchukua gari ili aende shamba na ghafla silaha aliyokuwa nayo ilidondoka na kufyatua risasi moja jambo lililozua taharuki kwa watu
"Mimi sina ugomvi wowote na mama na hizi taarifa ni za uongo, ukweli ni huo nilioueleza ndugu mwandishi, kwanza mama yangu mwenyewe hana silaha sasa nashangaa imekuwaje tukagombana na kufyatuliana risasi, kama ingekuwa adhma yangu ningelifanya tukio hili nyumbani sasa iweje ofisini? alisema John
"Kwanza mimi nashangaa hizi taarifa maana nilikuwa shambani baada ya kurudi nashangaa nakutana na waandishi wa habari wananihoju kujua kuhusu tukio hilo, na tayari pia taarifa zimeshazagaa kwenye mitandao ya kijamii, ndugu mwandishi huo ni uongo sijafyatuliana risasi na mama yangu" amesema
Hata hivyo Jonas Nkya ameongeza kwamba kilichojitokeza ni kuanguka kwa bastola yake iliyokuwa kiunoni, baada ya kwenda ofisi za faraja kubadilisha gari kwaajili ya kwenda shamba, ambapo ilijifyetua risasi mbili na kutoa mlio uliosababisha baadhi ya watu kusogea eneo hilo na kwamba kama kungekuwa na ugomvi wa kifamilia, ungefanyika nyumbani kwao ambapo yupo kwa sasa, akimsaidia mama yake kumuuguza baba yake Prof Nkya,ambaye amepooza, madai ambayo yameungwa mkono na mama yake mzazi ambaye naye amehojiwa katika ofisi za faraja, baada ya kukutwa akiendelea na majukumu yake.
Chanzo: ITV