Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
limewahamisha askari wake, WP 5863 Quine na WP 3548 Koplo Maeda kutoka
Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ilala kwa kukiuka maadili ya kazi.
Taarifa
ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao
Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema
askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea,
waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa
kufariki.
Kutokana
na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi
wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka
kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.
“Makosa
ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya
kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini
ya siku 30 na kadhalika,” lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa
polisi.
Chanzo:Mtanznia