Mchana wa saa tisa October 10 2014 Baba Levo ambae ni msanii wa bongofleva aliipigia simu millardayo.com
na kutoa taarifa za ajali aliyoipata saa saba mchana akitokea Tabora
kuelekea Mpanda ambako alikua anakwenda kwa ajili ya kutumbuiza.
Baba Levo anasema alizitoa hizo taarifa saa tisa mchana sababu ndio
aliweza kupata angalau network ya mtandao wa simu kwani kwa saa mbili
zilizopita alishindwa kupiga simu baada ya kupata ajali porini kutokana
na uzembe wa dereva wa Coaster aliehama upande wake na kuhamia upande wa
pili kukwepa barabara mbovu.
Kina Baba Levo walikua kwenye Basi kubwa lililogongana uso kwa uso na
Coaster hii ambapo Baba Levo alikua amekaa pale mbele pembeni kabisa ya
dereva kwenye kile kigodoro ambapo msanii huyu ilibidi akae hapo sababu
kiti chake kiliuzwa ticket kwa watu wawili hivyo aliamua kuiachia siti
yake kwa mama wa Kiarabu baada ya kujikuta wote wamepangwa siti moja.
Baba
Levo anasema japo taarifa za vifo hazijathibitishwa, kuna watu kama
Wanne ambao aliwaona wamepoteza maisha kwenye eneo la ajali kwa kupasuka
vichwa na viungo muhimu vya mwili.
Baada ya ajali hii kutokea, dakika zaidi ya 150 baadae ndio walipata
msaada na Baba Levo kwenda Hospitali kucheki afya yake ambapo
alisafishwa vidonda alivyoumizwa na vioo vilivyomrukia mwilini kama
inavyoonekana kwenye picha za hili basi hapa chini.
credits:millardayo.com