Mwili wa mshukiwa wa ujambazi ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuuaawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari
picha
ya juu na chini wananchi wa jiji la Arusha waliojitokeza kuuangalia
mwili wa marehemu huyo hatari aliouawa na polisi usiku wa kuamkia leo
wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa mtuhumiwa wa ujambazi nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha
baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa mtuhumiwa zikiwemo silaha mbalimbali
kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defence moja ambacho mtuhumiwa wa ujambazi alikuwa akikitumia.
Mshukiwa mmoja wa ujambazi aliyefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah alimaarufu kwa jina
la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuawa baada ya kupigwa
risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa
tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo October 10 mwaka huu majira
ya saa nane na dakika nne usiku katika kijiji cha Moivo kilichopo
ndani ya kitongoji cha Enaboishu wilayani Arumeru.
Alisema
kuwa marehemu Ramadhan Abdallh alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu na
jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo
yameshawahi kutokea ndani ya mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.
Alibainisha
kuwa kuuawa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na juhudi na kutumia mbinu za
kisasa za kiupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu)
ambapo askari polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi amri na
kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu
mashambulizi na kumsababishia umauti kumfika.
“Mara
baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa mwili wa
marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba
RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14)
ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi na
mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi
hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine
zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio
call moja yeye nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya toyo
power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU pamoja na
kofia ngumu”alisema Sabas
Aidha
alibainisha kuwa pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi
hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki
yenye namba za usajili T 805 CVD ambapo alibainisha kuwa jambazi hili
lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja na
chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla
yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola
pamoja na koti kubwa jeusi.
Kamanda
Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya
kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya saa tatu na
nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na mwenzake ambaye
ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina
la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingia
nyumbani kwake ,huku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00
maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki
walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea kichwani mototo
aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha
kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa
anapatiwa matibabu.
Kamanda
Sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi
nzuri pamoja na kuwaahidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na
kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.
“Arusha
sio sehemu ya kuhifadhi wahalifu hivyo tutajitaidi kwa hali na mali
kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na
napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga
vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia
waendelee kuwafichua wahalifu popote pale ili tuwaangamize
kabisa”alisema Sabas
Mmoja
wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo
Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro alilipongeza jeshi la polisi
kwa kuweza kumuangamiza jambazi huyo kwani limekuwa likiwatia mashaka
watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog