Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa.
Moja ya maduka ya vifaa vya pikipiki lililoteketea
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia tenki la lori hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya
kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga iliyopo Mbagala Rangi
tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la
mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta.
Mkuu wa Moa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32.
WATU
wa tatu wamefariki dunia huku wengine 16 wakijeruhiwa katika ajali ya
lori la mafuta lililopinduka katika mzunguko wa Mbagala Rangi tatu
jijini Dar es Salaa jana usiku.
Ajali
hiyo ya lori la mafuta ilitokea wakati lori hilo ambalo halijafahamika
ni mali ya kampuni gani kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulikwepa
gari lingine lililokuwa mbele yake.
Akisimulia chanzo cha ajali hiyo mmoja wa mashuda amesema mara baada ya
gari hilo kupinduka dereva alitoa tahadhari kwa vijana waliofika eneo
hilo kuwa waache kuchota mafuta hayo na endapo wakifanya hivyo
wathithubutu kuwasha moto au kugusa betri lakini ghafla palitokea mtu
aliyewasha mshumaa jirani.
Kuwashwa
kwa mshumaa huo kulisababisha moto kulipuka na hatimaye moto kufika
hadi katika gari hilo na kuunguza watu waliokuwa wakichota mafuta.
Mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta alikimbilia baa ya United State
kutafuta maji ajizime moto na kusababisha moto kulipuka tena eneo hilo
la bar na mtu mwingine alikimbilia eneo la gesti kutafuta maji nae
akasababisha moto katika magodoro na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ya
wageni iliyo na vymba 32.
Mbali
na nyumba hiyo ya wageni pia moto huo uliteketeza kabisa mali katika
vibanda vinne vya biashara vilivyokuwa eneo hilo na pikipiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic alifika katika eneio la
tukio na kutoa onyo kwa wananchi kusogelea magari ya mafuta yanapo
anguka.