Jeshi
la Polisi mkoani Tanga limewakamata kisha kuwatia mbaroni raia wawili
wa kigeni kutoka Nigeria wakiwa na zana za milipuko inayotumiwa katika
vitendo vya kigaidi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga kamishna msaidizi mwandamizi wa
Polisi Fraisser Kashai amesema watuhimiwa hao waliotambulika kwa majina
ya Kenneth Ekeneh Luodo na Amick Bonniface Aje ambao wamekamatwa katika
kijiji cha kigwasi kilichopo kata ya mashewa wilayani Korogwe ambapo
walikutwa kwa mwenyeji wao aliyetambulika kwa jina la Frank ambaye
alitoroka baada ya operesheni hiyo.
Amesema zana hizo ambazo pia hutumika kuvunja miamba na majengo
watuhumiwa walikuwa wamezihifadhi katika mabegi ndipo jeshi la Polisi
walipowakamata na kuwatia mbaroni kwa ajili ya upelelezi zaidi huku
jitihada za kumtafuta mwenyeji wao Frank zikiendelea.
Katika tukio lingine kamanda Kashai amesema mtu mmoja Michael
Charle amekamatwa akiwa na risasi 39 za silaha za kivita ambazo anadai
kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi kinyume cha taratibu ambazo
amedai kuwa ametoka nazo Monduli mkoani Arusha kwenda mkoani Morogoro.
CHANZO:ITV