Kuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama kukushtua kwa namna fulani.
Stori ambayo nimeipata hivi punde kutoka Kenya inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.

Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni
utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa
mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea
kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama
hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme
Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala
hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili
na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku
wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika kaonti ya
kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo
la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo