RAIS KIKWETE NA MAKAMU WA RAIS WAONGOZA WANANCHI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU WILLIAM SHIJA

Rais Jakaya Kikwete amewaongoza viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa pamoja na taasisi za kimataifa katika kuuaga mwili wa katibu mkuu wa kwanza mwafrika wa chama cha mabunge ya nchi wanachama wa jumuiya ya madola marehemu Dokta William Ferdinand Shija aliyefariki kutokana na ugonjwa wa saratani katika hospitali ya Charring Cross nchni Uingereza.
 
Akiwa ameambatana viongozi mbalimbali akiwemo makamu wa rais, Dokta Mohamed Ghalib Bilal, waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowasa pamoja na spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda katika viwanja vya Karim Jee jijini Dar es Salaam, rais Kikwete alipata fursa kuuga mwili wa marehemu Dokta William Ferdinand Shija na baada aliweka saini katika kitabu cha kumbukumbu.
 
Akiwasilisha salama za serikali, waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera utaribu na bunge, Mhe. William Lukuvi licha ya kumwelezea mareheu alikuwa mtaalamu aliyebobea katika fani ya uandishi wa habari pamoja na kuwa na uwezo mzuri wa lugha ya kiingereza amesema katika uhai wake alikuwa shupavu na mkweli na aliweza kushika wadhifa mbalimbali ndani ya serikali ikiwemo uwaziri katika wizara mbalimbali.
 
Rais wa tawi la chama cha mabunge ya nchi wanachama wa jumuiya ya madola kwa upande wa Tanzania, Mhe. Anna Makinda amesema marehemu dokta Shija alikuwa ni miongoni mwa wanaomani domokrasia ya vyama vingi sio upinzani au uadui bai ni changamoto za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi zaidi.
 
Marehemu dokta William Ferdinand Shija alizaliwa aprili mwaka 1947 na kufa Oktoba 2014 kwa maradhi ya kansa, amehacha mke na watoto watano,na mwili wake umesafirishwa leo kwa ndege kuelekea Sengerema mkaoni Mwanza kwa maazishi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mrisho Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 12, 2014. (Picha na OMR).
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mrisho Jakaya Kikwete, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mrisho Jakaya Kikwete, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mrisho Jakaya Kikwete, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
5B
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
6
Askari wa Bunge la Jamhuri, wakibeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee kwa ajili ya zoezi la kuagwa mwili, leo.
7
 Rais Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakijumuika na waombolezaji wakati wa zoezi la kuagwa mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, katika  Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
8
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wakiwa katika Viwanja vya Karimjee wakijumuika na waombolezaji wengine katika zoezi la kuagwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, leo.
9
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi waliohudhuria zoezi hilo la kuagwa mwili wa marehemu.
10
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo