Kioo cha lori cha
mbele kikiwa kimepasuka.
Makreti ya soda yalivyoanguka.
Baadhi
ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika
akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo.
Watu wakishuhudia ajali hiyo.
Chupa zikiwa zimeanguka kwenye mtaro.
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.
WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya
Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo
ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu,
mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia
ghafla mbele ya gari hilo kubwa
lililokuwa limebeba vinywaji na ndipo
gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)