MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YAMTOKEA PUANI MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, AMRI YA KUKAMATWA YATOLEWA

Na. Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Baraza la Maadili limetoa amri ya kukamatwa mara moja Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo kwa kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza hilo kujibu tuhuma zinazomkabili.
Akizungumza baada ya kuahirisha kikao cha Baraza hilo lililoanza vikao vyake tarehe 9/10/2014, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema kuwa amri hiyo imetolewa kwa mujibu wa fungu la 24 (4) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 ambayo imempa mamlaka Mwenyekiti wa Baraza hilo kutoa amri ya kukamatwa Kiongozi yeyote atakaekaidi wito wa kufika mbele ya Baraza na kwa mujibu wa fungu hilo amri hiyo itatekelezwa na Afisa wa Polisi.

Kiongozi huyo ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya Madaraka aliitwa mbele ya Baraza hilo ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.
Baraza la Maadili limeanza vikao vyake ambapo mashauri 19 ya viongozi wa kada mbalimbali wanaotuhumiwa kikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutumia vibaya madaraka yao na kushindwa kuwasilisha Tamko la Mali na Madeni yatasikilizwa.

Vikao hivyo vya Baraza la Maadili vinafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya Viongozi husika.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Baraza hilo litaendelea na vikao vyake mpaka tarehe 17/10/2014.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjai634a4MeKvbE-mZhvx3RAgFfChH_tXnw_z5IyAF-JtfTxr4iuQI65q70a_EYznoLj-UJirxlS7Kj0DlYsFomoHtLbtfy-yBc3f6v-u0cp9v59cHcKWHFXhHxj1m9j2sVf_jCrehzjI3d/s1600/unnamed+(27).jpgMwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi katikati akiwa na Wajumbe wa Baraza hilo Bibi Selina Wambura kushoto na Bibi Hilda Gondwe kulia kabla ya kuanza kusikiliza Mashauri ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXaTGNgpGdyI3Kc9vLrrc0t56gySiMb4qGbeqfBfUF4QD4vO-AEg593XJQBft58RT9gdVN-H2Si-4sOegaMCosk_zWk8hXLbhCDlq43E1Bf_bDfMTgGGDA1Bv4VzeftrSfEiXTs5cSfui4/s1600/unnamed+(28).jpgMwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Hassan Mayunga akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Jaji Hamis Msumi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo