NEWS ALERT: UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA



 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto) akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
Baadhi  ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na waandishi  wa habari kuhusu  taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akijadiliana  jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi,  Julias Malaba (kulia) baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.
Baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) wakifuatilia mkutano huo.picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo.
Kitendawili cha tarehe rasmi ya Watanzania kupiga Kura ya Maoni itakayopitisha au kukwamisha Katiba Inayopendekezwa, kitateguliwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec) baada ya kukamilisha uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapigakura Aprili mwaka ujao.
Nec imebainisha hayo jijini Dar es Salaam jana ikieleza kuwa  tayari Serikali imetoa Sh15 bilioni za uboreshaji huo na kwamba utakamilika Serikali itakamilisha kutoa Sh270 bilioni zinazohitajika kwa ajili ya uboreshaji wa daftari hilo.
Hadi sasa, kuna mkanganyiko kuhusu tarehe hiyo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutaja mwezi Aprili  mwakani kama wakati wa kupiga kura hiyo, akipingana na Machi 15 iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema. 
Makamu mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa tume hiyo itakamilisha daftari hilo ifikapo Aprili mwakani.
‘’Mpaka sasa Serikali   imeshatoa Sh15 bilioni, tutaendelea kupokea kidogo kidogo kutoka Hazina. Ikiwa zikifika kwa wakati, tutakamilisha zoezi hili Aprili 18 mwakani,’’ alisema na kuongeza: ‘’Mtakumbuka awali tuliarifu wananchi kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura lingeanza Septemba mwaka huu, hata hivyo halikuanza kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha kutoka serikalini.’’
Alisema kuwa kwa sasa Nec imeanza kupewa fedha na Serikali  kuwawezesha kuanza kwa zoezi hilo la uboreshaji daftari hilo.
Jaji Hamid aliongeza kwamba mara baada kupokea kiasi hicho pamoja na vifaa vya uboreshaji wa daftari hilo, Nec ilianza kutoa mafunzo kwa watendaji wake.
“Novemba mwaka huu, tutafanya majaribio ya uboreshaji daftari la wapigakura kutumia mfumo wa ‘Biometric Voter Registration’ katika majimbo matatu ya uchaguzi ya Kawe Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele Halmashauri ya Mji wa Katavi,” alisema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo