Kuna taarifa zilitoka leo jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa
na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram
Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
Imefahamika ni kweli
msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea
uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba
dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati
lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye
mahojiano na millardayo.com kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika viwanja vya ndege Tanzania
amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii huyu alipohojiwa
amekiri kweli kuwa dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya
safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua
zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko
na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni
kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya
kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kuusikiliza hapa.
chanzo:millardayo.com