Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha mchoro wa
reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango vya kisasa
wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China yakiongozwa
na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim Bank,
China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt.
Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya
China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake kuhusu
mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya
kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua
kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko
Beijing tarehe 24.10.2014.PICHA NA JOHN LUKUWI.