Mahabusu aitwae Andaluswe Mwakapila mkazi wa Olongo Mbeya amejinyonga
na kufariki dunia akiwa ndani ya mahabusu katika kituo kidogo cha
Polisi Inyala ambapo Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi alithibitisha
kutokea kwa kifo hicho na kusema mwili wa marehemu ulikutwa
unaning’inia katika dirisha la chumba cha mahabusu.
Alijinyonga kwa kutumia shati lake ambapo chanzo cha kujiua
inasemekana kabla ya kufikishwa mahabusu alikua na ugomvi na mkewe
ambapo alimpiga kwa kutumia shoka na jembe na kumsababishia majeraha
mengi.