MTOTO ANYWA SUMU BAADA YA KUNUSURIKA KUBAKWA NA BABA YAKE MZAZI HUKO TANGA

Jeshi la Polisi Tanga linamshikilia mtoto mwenye miaka 16 kwa kosa la kunywa sumu kwa lengo la kujiua baada ya kunusurika kubakwa na baba yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Tanga Frasser Kashai alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 18 mwaka huu wakati baba yake Richard Leornad alipomvamia kwa lengo la kutekeleza ubakaji huo lakini mtoto huyo alifanikiwa kumtoroka na kuokolewa na wasamaria wema.

Alisema kwa sasa mtoto huyo anatibiwa katika hospitali ya Bombo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi huku baba yake huyo akishikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo