Ni
pale ambapo unaweza kuvuta picha baba anajaribu kufanya mbinu za
kumsafirisha mtoto wake kwenda nchi ya pili ili akamuuze kwa watu ambao
ameshazungumza nao kabisa na wako tayari wanasubiria biashara ifanyike.
Yani hiki kisa kilichotokea Kenya kina uzito wake mpana tu sababu
Baba mzazi na Baba wa kambo wote wamehusika kwa nyakati tofauti kufanya
mbinu za kutaka kumsafirisha mtoto huyu ambae ni Albino ili aje Tanzania
kuuzwa na viungo vyake vitumike kwa imani za kishirikina.
NTV wameripoti kwamba Polisi wa
Kenya ndio walimuokoa huyu mtoto akiwa tayari ameshaingizwa Tarime
Tanzania akiwa anasafirishwa kwa siri na baba yake wa kufikia (wa kambo)
ambapo mama mzazi amesema baada ya kuolewa na mume wa pili baada ya
kuachana na yule wa kwanza ambae ndio baba wa mtoto, amekutana na kitu
kilekile kama alichotaka kufanya mume wa kwanza, mume wa pili pia
anataka kumuuza huyu mtoto.
Mama wa mtoto anasema ‘ninachoshangaa ni kwamba baba yake mzazi
alipotaka kumuuza huyu mtoto alikamatwa, tena baba yake wa pili
amejaribu kuja kutaka kuiba tena huyu mtoto, ni giza ambalo nimeliona
kwangu na kuhofia maisha ya mtoto na mpaka sasa tunamfungia ndani hawezi
kutoka hata kwenda shule’
Kwenye sentensi nyingine mama wa mtoto huyu anasema ‘Wakati
mwingine najiuliza kwa sababu baba yake mzazi wa kwanza alishikwa na
Polisi lakini sijui hiyo kesi iliendeleaje na akaachiliwa, sasa ni kama
wameona ni kawaida hata kama wanakwenda kuripotiwa hakuna hatua yoyote
inachukuliwa kuhusu huyu mtoto’
CREDITS; millardayo.com