Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa
Habari wa taasisi hiyo, Patrick Mvungi, alisema ajali hizo
zinasababishwa na madereva pamoja na abiria kushindwa kuvaa kofia ngumu
pindi wanapokuwa barabarani.
Mvungi, alisema taasisi hiyo ikiwa katika kipindi cha mpito cha
mageuzi ya utoaji huduma za afya nchini, imefanikiwa kwa asilimia 95
kutoa huduma muhimu za tiba na upasuaji kwa wagonjwa na hivyo kupunguza
vifo na rufaa za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi.
Alisema zaidi ya wagonjwa 4,500 wa mifupa wamepatiwa huduma kwa
kutumia utaalamu wa kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum (Sign
Nail), kwa wagonjwa waliovunjika mifupa kinachowasaidia kupona mapema
na kurudi katika hali zao za kawaida.
“Kwa upande wa Upasuaji Mkubwa wa Nyonga (Total Hip Replacement),
zaidi ya wagonjwa 1,256 walipasuliwa salama na wamepona, huku zaidi ya
wagonjwa 703 wakifanyiwa upasuaji mkubwa wa kubadilisha viungo vya goti
vilivyoharibika (Total Knee Replacement), kwa kuweka vifaa maalum vya
bandia (Artificial Implants), ambapo zaidi ya 95 ya wagonjwa wameweza
kutembea na kurudi katika hali zao za kawaida,” alisema.
Mvungi, alisema taasisi hiyo pia imefanikiwa kutoa matibabu kwa
wagonjwa ya ubongo (Brain Surger diseases), waliokuwa wakihitaji
upasuaji kwa zaidi ya asilimia 80.
Na
Janeth Jovin