MAJERUHI WA AJALI YA BASI LA MWAFRIKA MKOANI NJOMBE WAZUNGUMZIA KILICHOTOKEA


Jumla ya Majeruhi 32 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe ya Kibena Wakipatiwa matibabu kufuatia kutokea kwa ajali ya gari la Kampuni ya Mwafrika iliyotekea leo majira ya saa nne asubuhi wakati basi hilo likitokea Wilayani Makete kuelekea Mkoani Iringa.

Wakizungumza nasi Baadhi ya Majeruhi wa Ajali hiyo wamesema kuwa Aajali hiyo imetokana na Mwendokasi wa dereva  wa gari hilo Ambapo wamesema alijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake  Jambo ambalo limesababisha kuacha njia na kuingia kwenye mtaro wa maji na kusababisha majeruhi hao.

Aidha Majeruhi hao wamesema basi hilo lilikuwa likitokea Wilayani Makete likielekea Mkoani Iringa limesababisha Majeruhi Mbalimbali Wakiwemo walikuwa wakitokea katika Hospitali ya Ikonda baada ya kupata unafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani  na kukutwa na ajali hiyo.
 

Mganga  Mfawidhi wa Hospitali ya Kibena Dr Patrick Msigwa  Amesema kuanzia majira ya saa nne na nusu wameanza kupokea majeruhi Ambao wamefikia idadi ya watu 32 waliojeruhiwa Ambapo hadi sasa majeruhi watatu wameruhusiwa kwenda katika hospitali ya Ikonda kuendelea na matibabu.

Kamanda wa  Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa  Ajali hiyo na kusema kuwa  Gari la Kampuni ya Mwafrika lenye Namba  za Usajiri T 726 AGA aina ya Scania  liliacha njia na kuanguka na kusababisha majeruhi hao katika eneo la mashamba ya chai Kibena.

Kamanda Ngonyani amesema Majeruhi Watatu wameruhusiwa kwenda Nyumbani Ambapo wengine bado wapo katika Hospitali ya Kibena wakipatiwa Matibabu na kuwataja Majeruhi Wawili waliozidiwa   kuwa ni pamoja na Aidan  Sekrand 72 Mkazi wa Makete ambaye amevujika mikono yote miwili na Janne  Chengula  49 Mkazi wa Makangalawe Wilayani Makete aliyevunjika mkono mmoja mara tatu.

Kufuatia Kutokea kwa ajali zinazosababishwa na Uzembe wa Madereva wa Vyombo vya Moto Kamanda Ngonyani ametumia Fursa hiyo kuwataka madereva wote kutii sheria bila shuruti kwa kupunguza Mwendokasi wakiwa barabarani ili kupunguza Ajali zisizo za lazima.


Picha hii ni ya majeruhi na si nzuri sana kuiangalia, ukitaka kuiona bonyeza hapa

Na Michael Ngilangwa, Njombe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo