Mratibu wa Makaburi na Mazishi Dar es
Salaam Nasibu Rashid amesema jiji la Dar es Salaam huzika wastani wa
maiti 15 zisizokuwa na ndugu, vichanga waliofariki baada ya kuzaliwa, au
wasiokuwa na uwezo kufanya mazishi kila mwaka, ambapo kwa mwezi
wamekuwa wakizika maiti kati ya 30 na 40.
Amesema maiti wanazozika zinatoka
hospitali ya taifa Muhimbili, Mwananyamala, Temeke, Ocean Road, Amana,
Vijibweni, na nyingine kutoka Zahanati za Manispaa za jiji ambapo maiti
hizo ni zile zilizokaa hospitalini kwa zaidi ya wiki 2.
Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Manispaa
ya Kinondoni amesema maiti nyingine zinazozikwa zinaletwa na jeshi la
polisi kutokana na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.