Mwakilishi wa kike wa Tanzania, Laveda ameondolewa kwenye mashindano ya Big Brother Africa Jumapili hii.
Laveda
amekuwa mshiriki wa sita wa kike kuondolewa kwenye mashindano hayo.
Mshiriki mwingine aliyetoka leo ni Alusa wa Kenya ambaye amekuwa
mwanaume wa kwanza kutoka. Kenya haina tena mwakilishi kwenye shindano
hilo.
Tanzania imebakiza mshiriki mmoja, Idris Sultan.