Timu ya Vijimambo inamasikitiko makubwa ya habari ya upotoshaji iliyoandikwa na gazeti la Jamhuri lililobeba kichwa cha habari "AUNTY EZEKIEL ATANUA NA WAZIRI NYALANDU MAREKANI" yakiwemo
magazeti mengine yaliyodandia kuandika habari hii bila kujua ukweli upo
wapi. Timu ya Vijimambo ikiwemo kamati ya maandalizi imechukizwa sana
kwa Gazeti hili kuandika habari ya kizushi na inayojeruhi hisia ya
familia ya Mhe. Waziri Lazaro Nyalandu kwa makusudi.
Habari hii ni uongo ulioandikwa kichochezi na mwandishi anayeitwa Alfred
Lucas. Timu ya Vijimambo haikufurahishwa na uongo huu pamoja na VIJIMAMBO BLOG kuwa ndio wahusika wakuu, mwandishi alitakiwa kutupigia simu ili aweze kupata habari ya upande wa pili.
Masanja Mkandamizaji na Shilole walipokuja mwaka 2013 kwenye sherehe
ya miaka 3 ya Vijimambo iliyobeba ujumbe wa Tamasha la Utamaduni wa
Kiswahili
Kwa kumsikiiza Aunty Ezekiel mwenyewe anasemaje kuhusu habari hii kama anavyoripoti Mubelwa Bandio wa Kwanza Production bofya play
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wakiwemo wadau wa Kimarekani wanaotangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani. Mhe. Lazaro Nyalandu alikutana na wadau wa Utalii siku ya Ijumaa Sept 12, 2014 kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na wadau walipomueleza Mhe. Waziri dukuduku lao na changamoto wanazokabiliana nazo wanapowapeleka Watalii Tanzania.
Katika gazeti hilo pia limeandika "Aunty Ezekiel amekaa Marekani siku 14" Ndugu
mwandishi Aunty Ezekiel amekaa Marekani siku 10 tu amekuja Sept 13,
2014 na ameondoka Sept 24, 2014 na Aunty Ezekiel hakuja kupumzika huku
na Waziri kama ulivyopotosha na uandishi wako wa uchochezi, uliojaa
chuki na husda kama nilivyosema hapo awali kwamba Aunty Ezekiel ameingia
Marekani siku ya Jumamosi Sept 13 na Mhe. Waziri Lazaro Nayalndu
ameingia Marekani siku ya Ijumaa Sept 12, 2014. Aunty Ezekiel na msanii
mwingine wa Bongo Flava Kassim Mganga safari zao zimeratibiwa na Kamati
nzima ya Vijimambo kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani na Jumuiya ya Watanzania DMV huku wakiwezeshwa
na wadhamini mbalimbali waliojitokeza kudhamini tamasha hilo la Utalii.
Wenyeji wa wasanii hawa walikua timu ya Vijimambo pamoja na kamati yake.
Lengo la wasanii hawa kama walivyokuja wasanii Masanja Mkandamizaji na
Shilole ni kuonyesha utamaduni wetu na Utalii kupitia soko la wasanii wa
Tanzania ikiwemo kuwatangaza wasani wetu kimataifa.
Waziri Lazaro Nyalandu akizindua kampuni ya Utalii Sept 16, 2014
jimbo la California kampuni inayomilikiwa na Balozi wa heshima Ahmed
Issa.
Ndugu mwandishi Aunty Ezekiel na Waziri wameonana mara moja tu usiku wa
Sept 13, 2014 kwenye kilele cha sherehe ya Utalii na baada ya hapo
hawakuwahi kuonana tena na baada ya sherehe ya Utalii Jumatatu Mhe.
Waziri Nyalandu alisafiri kuelekea California kuzindua kampuni ya Utalii
ya Tanzania Safari and Tourism inayomilikiwa na Balozi wa Heshima Ahmed
Issa na hakuwahi kurudi tena Washington, DC mpaka siku aliyoondoka.
Msanii Shilole akimsalimia Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwnyi
alipokuja mwaka 2013 kwenye Tamasha la utamaduni la Kiswahili nchini
Marekani.
Ndugu mwandishi sababu iliyomleta Mhe. Waziri nchini Marekani ni
kutokana na ujumbe wa Utalii na kukemea ujangili na Mhe.. Lazoro
Nyalandu ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kama ilivyokua kwa Rais Mstaafu Ali
Hassan Mwinyi alipokua mgeni rasmi kwenye tamasha la Utamaduni la
Kiswahili.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknologia Mhe. January Makamba na mkewe
wakiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles huku wakipokelewa na
Afisa Mindi Kusiga wakati huo akiwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,
kushoto ni Mwenyekiti kamati ya Vijimambo Bw. Baraka Daudi.Mhe.
Janauary Makamba alikua mgeni rasmi wa sherehe ya Uhuru miaka 51.
Tunaiomba Serikali kuyachukulia hatua zinazositahili magazeti kama haya
yanayoweza kujeruhi hisia ya mtu na habari ya uongo kama hii ni sumu
kubwa kwenye mahusiano na upendo kwa familia na siku zote habari ya
uongo hua na nguvu kuliko ukweli.
Mwisho timu ya Vijimambo na kamati ya maandalizi tunaomba radhi kwa Mhe.
Waziri Lazaro Nyalandu kwa usumbufu na maumivu ya gazeti la Jamhuri na
magazeti mengine yaliyodandia habari yalivyosababisha kwako na familia
yako. Siku zote tutakua mstari wa mbele kufanyakazi na wewe popote na
wakati wowote.
Aunty Ezekiel akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania
Umoja wa Mataifa New York, kulia ni Balozi Tuvako Manongi Balozi wa
Tanzania Umoja wa Mataifa.