KUHUSU KIWANDA CHA MAFUTA KUTEKETEA KWA MOTO HUKO SINGIDA


Maghala matano ya kiwanda cha Maunt Meru Oil Miller cha mjini Singida kimeteketea kwa moto na kuunguza zaidi ya tani elfu tatu za mashudu ikiwemo mashine ya kukamulia mafuta na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Akieleza mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone amesema   kiwanda hicho ambacho kimeanza kuungua majira ya saa tano usiku wa tarehe ishini natatu hadi sasa,imebidi mkoa kuomba gari lingine kutoka mkoa wa jirani wa manyara ili kuweza kusaidia kuzima moto ambao bado unaendelea kuwaka.
 
Kwaupande wake kamanda wa polisi mkoa wa singida  kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Bwana Thobias Sedoyeka amethibitisha kuungua kwa kiwanda hicho na  jeshi la polisi limejitahidi kuweka ulinzi  na  amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi matukio kama hayo yanapo tokea.
 
Meneja wa kiwanda hicho Bwana Sajay Sumarzya  amesema wao walipata taarifa kutoka kwa walinzi usiku majira ya saa tano  na walipo fika walikuta maghala matano ya mashudu  yenye tani zaidi ya elfutatu  yakiwaka moto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo