Shirika la afya duniani WHO
linasema kwa msichana wa umri wa miaka miwili ambaye alithibitishwa kuwa
mgonjwa wa kwanza wa ebola nchini Mali alisafiri kilomita kadha kwa
basi nchini humo huku akionyesha dalili za kuugua ugonjwa huo.
Zaidi
ya watu 40 ambao walikaribiana naye wametengwa. Huenda msichana huyo
alisafirishwa kwenda nchini Mali na nyanyake baada ya mazishi ya mamake
nchini Guinea moja ya nchi ambazo zimeathirka pakubwa na ugonjwa wa
ebola.
Utawala nchini Mali sasa umethibitisha kuwa msichana huyo
ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Mayes alikokuwa akipewa
matibabu.
Mwandishi wa BBC anayehusika na masuala ya afya anasema
kuwa huenda ikawa changamoto kubwa kuwapata watu wengine ambao
walikaribiana na msichana huyo.