KAULI YA AUNT EZEKIEL KUHUSU TETESI ZA KUTOKA KIMAHABA NA WAZIRI NYALANDU




Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.
 
Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.

“Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo