Kila mmoja amekua na hofu akisikia au kukutana na mtu alietoka kwenye
nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola barani Afrika na ndio maana
ubaguzi umeripotiwa katika nchi mbalimbali za Amerika, Ulaya na hata
Afrika ikijulikana unatokea Afrika.
Ripoti mpya inasema Mwanamke mmoja wa Kenya amefia kwenye uwanja wa
ndege Jomo Kenyatta Nairobi kwa tetesi kwamba alikua anaumwa Ebola au
Marbug ambapo familia yake imeilaumu Serikali kwa kifo cha ndugu yao kwa
kutelekezwa na wauguzi kwenye Clinic ya uwanja wa ndege waliokua na
hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola.
NTV Kenya wameripoti kwamba
Marehemu ambae alikua mfanyabiashara aliondoka nchini Kenya na kuelekea
Juba Sudan ambapo alipitia Uganda wakati mlipuko wa Marburg ulipotokea
na alipowasili Juba alikua anavuja damu kwenye sehemu ya uzazi jambo
lililofanya dada yake amrudishe Nairobi kwa ajili ya matibabu.
Baada
ya ndege kutua tu Familia yake inasema hakuhudumiwa ipasavyo ambapo kwa
muda wa dakika 120 Mama yake mzazi na rafiki yake walibaki kutazama tu
hali yake ikiendelea kudorora na alikua akilalamika anaumwa kichwa na
amemiss mtoto wake wa kiume.
Mama Wanjiku pamoja na rafiki yake pamoja na Marehemu waliwekwa
kwenye chumba kimoja kwa zaidi ya saa tano kabla ya kuruhusiwa kuondoka
ambapo Wanjiku alifariki dunia akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Mama mzazi na rafiki yake waliruhusiwa kuondoka kabla ya matokeo ya
uchunguzi wa matibabu kutolewa, kama Marehemu alikua akiugua Ebola au
Marburg basi kuachiliwa kwao kungepelekea kusambaa kwa ugonjwa huo kwa
haraka….