Idadi
ya watu waliopoteza maisha kwa ajali ya moto uliosababishwa na watu
waliokuwa wakiiba mafuta ya petroli baada lori lililobeba shehena ya
mafuta hayo kuanguka karibu na makazi ya watu eneo la mbagala Charambe
jijini Dar es Salaam imeongezeka na kufikiwa watano.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa uhusiano wa hospitali ya
taifa ya Muhimbili, Bi Doris Ishinda amesema vifo vya wagonjwa wawili
zaidi vimeongezeka jana jioni na usiku wa kuamkia leo na kufanya idadi
ya wagonjwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mpaka sasa kuwa kumi
na moja.
Aidha katika hospitali ya Temeke wagonjwa wanne wanaendelea kupata
matibabu na kufanya idadi ya wagonjwa waliolazwa mpaka sasa kupungua
hadi kufikia 15 katika hospitali ya Temeke na Muhimbli na vifo
imeongezeka toka vifo vitatu hadi vitano.