Wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiangalia chanzo cha chemichemi ya maji cha Ikorongo kilichoko kilometa 13.2
kutoka Mpanda mjini. Chanzo hicho kina uwezo wa kutoa maji ya kutosha mji wote
wa Mpanda.
Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Magdalena Mkeremi
(aliyejifunika mtandio) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi Rais, Tume ya Mipango walipotembelea chanzo hicho hivi
karibuni
Mhandisi
Happiness Magalula, Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na
Huduma (mwenye sweta la blue) akitaka ufafanuzi wa miundombinu ya kuwezesha
maji kuwafikia wananchi kutoka katika chanzo hicho. Bomba la inchi kumi
limetandazwa kutoka kwenye chanzo hicho mpaka mjini ambako kuna tanki kubwa la
maji yanayosambazwa katika mji wa Mpanda na vitongoji vyake
Tanki
la maji lenye uwezo kujaza lita 1,000,000 linalosambaza maji katika mji wa
Mpanda, mkoani Katavi
Moja ya
bomba la maji katika shule ya Sekondari ya Shanwa katika mji wa Mpanda ambao
wanapata maji kutoka katika chanzo cha maji cha Ikorongo. Anayefungua bomba ni
Festo Katanti, Mtalaam wa maji wa Halmashauri (Techenician) nyuma yake ni
mwalim Mkuu wa Shule hiyo Emmanuel Nkumbo na kushoto kwa Katanti ni Mhandisi
Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango.
Na
Mwandishi wetu, Katavi
Chanzo cha maji cha chemichemi
ya Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini, mkoani
Katavi. Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa asili unaolinda
maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa
Katavi Magdalena Mkeremi anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji
masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi. Chanzo hiki kina uwezo wa
kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.Mradi wa maji wa Mji wa
Mpanda ni wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote bali maji
husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).
Bomba kubwa la maji la
inchi kumi limelazwa kutoka kwenye chanzo na kupelekwa Kazima kwenye tanki
kubwa la ujazo wa lita milioni moja ambalo limejengwa eneo la kilometa 13
kutoka kwenye chanzo cha maji. Vile vile
maji kutoka kwenye tanki hilo na kwenda
mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko hivyo, kurahisisha gharama
zake.
Mradi huo wa maji wa vijiji
kumi au mitaa kumi ya mji wa Mpanda unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa. “Maji yalikuwa tatizo kubwa
hapa kwetu lakini ujio wa mradi huu umerahisisha upatikanaji wa maji mjini na
kwenye mitaa ya mji wa Mpanda,” anasema Mhandisi.
Tayari vimejengwa vituo vya
kuchotea maji 41 katika mitaa kumi na watu binafsi wapatao 300 wameunganishiwa
maji kupitia chanzo hicho cha maji. Amesema mradi huo umetekelezwa
kwa muda wa miaka mitatu tangu 2012/13 -2014/15 ambapo umekamilika mwezi
Septemba 2014.Amesema ili kuufanya mradi
huo kuwa endelevu wamejenga nyumba ya mlinzi ili kulinda chanzo hicho cha maji
kisiharibiwe kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira
yanayozunguka eneo hilo.