Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo
yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo
imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa
ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa
matukio hayo.
Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News
inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu
jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi
la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Akitoa taarifa za kifo cha mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha Lebaratus Sabas amesema marehemu yahaya hassan omari hela maarufu kwa jina la (sensei) ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikamatwa wiki mbili zilizopita mkoani morogroro na kupelekwa arusha na bado alikuwa anaendelea kuhojiwa.
Kwa mujibu wa kamandaa sabas mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa marehemu yahaya, alikiri kuwa yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa matukio yote ya milipuko ya mabomu na ya kumwagia viongozi wa dini tindikali yaliyowahi kutokea mkoani arusha na maeneo mengine.
Aidha kamanda Sabas Amefaanua kuwa baada ya marehemu ambaye ni mtuhumiwa kukiri tuhuma hizo alikuwa bado anaendelea kutoa ushirikiano kwa kuanza kuonyesha vitendea kazi yakiwemo mabomu ambayo alidaiwa kuyaficha kondoa mkoani Dodoma.
Amesema wakati anasafirishwa walipofika eneo la kisongo katika barabara kuu inayoenda dodoma majira ya usiku alifanya jaribio la kutaka kutoroka na ndipo akapigwa risasi iliyomjeruhi mguu na kiuno na akafariki wakati anapelekwa hosipitali.