Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Watanzania wametakiwa kuchagua viongozi
wanao faa na wenye kupenda maendeleo katika jamii pasipo kuangalia sura
wala wasifu wa mtu katika chaguzi zijazo.
Hayo yalisemwa jana na Dr Moses Mgara
katka mkutano wa hadhara wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
uliofanyika katika viwanja vya Isansya Wilayani Mbozi Mkoani
hapa,alisema maendeo mengi yanashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na
Watanzania kuwachagua Viongozi wasiokuwa na mapenzi bora na Wananchi
wao bali wanakuwa na hutu na madaraka.
Dr mgara aliendelea kwa kusema kuwa
Desemba mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa hivyomuafaka
wa Watanzania kuchagua Viongozi wanaofaa kwa kuongoza kwa miaka mitano
na wapenda maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa chama cha walemavu
Wilayani mbozi ambaye pia ni katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Amina
Solar amewasihi Wanawake kujitokeza kwa wingi ilikuwania nafasi za
Uongozi ili kuleta mabadiliko katika jamii husika
Pia alisema kuwa kumekuwa na changamoto
nyingi zinazowakabili katika jamii na ambazo hazijafanyiwa ufumbuzi
kutokana na uchache wa wanawake wanaojitokeza kuwania nafasi za uongozi
,hivyo kuwasihi kujitokeza kwa wingi ili kuwania uongozi na kuleta
mabadiliko.
Akimalizia Mkazi wa Kijiji cha Isansya
Acksoni Ryanda aliwasihi viongozi watakao Chaguliwa kutekeleza ahadi zao
za maendeleo kwa muda muafaka na si kusubiri kipindi cha uchaguzi na si
wananchi kuishi maisha ya shida.
