Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
(CREDIT: BBC SWAHILI)