Mwanamke afia kwa hawara, Mwanaume ahaha na kueleza ukweli wa mapenzi yao

MWANAMKE Jane Bhoke (27) amefariki dunia nyumbani kwa hawara yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kifo hicho kilitokea juzi saa 12 jioni eneo la Zingiziwa Chanika wilayani Ilala.

Kamanda Nzuki alisema mtoa taarifa, Mohamed Kambi (44) mkazi eneo hilo alieleza kwamba alikutana na marehemu Septemba 12 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji huko Chanika.

Kambi alisema baada ya kukubaliana walianza kuishi kama mke na mume na huku akibainisha kwamba walifanya mapenzi mara mbili.

“Septemba 15 saa 11 jioni mtoa taarifa na marehemu walikwenda magengeni kununua mahitaji ghafla marehemu alianguka akawa analalamika mguu wa kulia unamuuma… katika harakati za kupunguza maumivu alimeza dawa aina ya diclopa,” alisema kamanda.

Alisema hali ya mgonjwa haikubadilika na ilipofika Septemba 16 saa 10 jioni alifariki dunia huku akibainisha kwamba haifahamiki marehemu ni mkazi wa wapi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo