Rai hiyo imetolewa na meneja Uendeshaji wa Benki ya wananchi Njombe ya NJOCOBA bwana Alex chizalema Akiwa Mgeni rasmi kwenye mahafari ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Luhuji.
Bwana chizalema amesema kuwa wazazi wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuwasomesha watoto wao kwaajili ya manufaa yao kwani wasipo soma taifa litaendelea kuwa na ongezeko la watoto wa mitaani na vijana wasiokuwa na ubunifu wa kufanya kazi.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa halmashauri ya Mji wa Njombe Shegeli Shengeli,Afisa elimu Ufundi wa halmashauri hiyo bwana Said Ibwe amesema amesikitishwa kupewa taarifa ya baadhi ya wazazi ambao wamehusika kutorosha watoto wao wasifanye mtihani wa darasa la saba mwaka huu.
Bwana Ibwe Amemuagiza mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Luhuji kutopeleka cheti cha mtoto huyo Nakwamba halmashauri kupitia idara ya Elimu itawafuatilia wazazi waliohusika kutorosha watoto wasifanye mitihani pamoja na kuwafundisha wafanye vibaya.
Awali akitoa taarifa fupi ya shule Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Luhuji bi.Grace Mrwillo Amesema kuwa kati ya wanafunzi 87 mwanafunzi mmoja James Thomas Mlelwa ameshindwa kufanya mtihani huo baada ya wazazi wake kumtorosha dakika za mwisho.
Na prosper mfugale