RB namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar, imemtia
mbaroni mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na
mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua
mhudumu wa baa aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu anayetuhumiwa kumshambuli mhudumu wa baa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha
lilijiri wiki iliyopita kwenye baa maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta,
Dar.
Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa
alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na
kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na
alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Mhudumu wa baa anayetambulika kwa jina la Aika Andrew (32) aliyenusurika kuuawa na mtangazaji maarufu Bongo, 'Lady Hanifa' .
Kwa mujibu wa mashuhuda, katika tukio hilo lililojiri mishale ya saa
11:00 jioni, Hanifa alipofika aliingia moja kwa moja jikoni kuangalia
biashara yake kisha akarudi kukaa sehemu ya baa.
Ilisemekana kwamba
Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu
ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona
kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu.
Majeraha ya moto shingoni mwa Aika Andrew.
Ilidaiwa kwamba alimwita mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha
aliyokuwa akidai Aika lakini muda huohuo Lady Hanifa akaanza kudai
chenji yake kwa mabavu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Wasamaria wema wakimpeleka Hospitali ya Mwananyamala, Aika Andrew.
Iliendelea kudaiwa kwamba katika
purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu alimchoma nacho Aika
tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa akimuunguza shingoni kwa
kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya moto kisha wakakimbia.
Habari zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia
Kituo cha Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema
walifika katika kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu
mwili mzima.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
CREDITS:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi