Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili mkazi wa Uzunguni jijini Arusha, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Hoteli Diamond Motel iliyopo eneo la Sakina jijini hapa.
Mwili wa mfanyabishara huyo anayemiliki mali
mbalimbali ikiwamo mgahawa wa Bite Bite na duka maarufu la vinyago eneo
la Kisongo uligundulika jana saa 7:00 mchana, wakati wahudumu wa hoteli
hiyo wakitaka kufanya usafi chumba alichokuwa amepanga.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri unaokadiriwa
kufikia miaka 56 , ilidaiwa aliingia hotelini hapo na mwanamke mmoja
ambaye hata hivyo, haikujulikana muda ambao alitoka.
“ Metili (Marehemu) alifika katika hoteli hiyo
akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika na kuingia
katika chumba chake na haijulikani aliondoka muda gani huyo mwanamke,”
alisema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas
hakupatikana jana kuelezea taarifa za awali za uchunguzi wa kifo hicho,
lakini maofisa wa polisi waliuchukua mwili huo, wakisema huenda kesho
taarifa itatolewa rasmi.
Tukio hili, linakumbusha kifo cha Kada wa CCM,
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa, Benson Mollel ambaye
alifariki dunia katika hoteli ya Lash Garden eneo la Jakaranda ambapo
pia alidaiwa aliingia katika chumba hicho na mwanamke.
Matukio ya kufa katika nyumba za wageni, katika
jiji la Arusha, yanahusishwa na matumizi ya pombe kali au dawa za nguvu
za kiume kwa wanaume wengi ambapo dawa zimekuwa zikiuzwa katika maeneo
mengi jijini hapa bila ya udhibiti mkali
