MAANDAMANO YA CHADEMA YAGONGA MWAMBA SHINYANGA,VIONGOZI WAKE WAJIFICHA,WAFUNGA OFISI

Hivi ndivyo jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limejipanga kukabiliana na maandamano yaliyotangazwa na Chadema jana ya kupinga bunge la katiba ambayo yalitarajiwa kufanyika kuanzia leo saa mbili asubuhi lakini mpaka sasa hakuna kiongozi wa chama hicho aliyejitokeza,hata ofisi ya Chadema imefungwa
Ofisi ya Chadema mkoa wa Shinyanga ikiwa imefungwa
 Askari wakiwa mtaani
 FFU wakiwa mtaani kukabiliana na waandamanaji kama watajitokeza leo.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Maandamano yaliyotangazwa na Chadema mkoa wa Shinyanga yaliyopangwa kufanyika leo saa mbili asubuhi,yameishia pasipojulikana baada ya viongozi wa Chama hicho kufunga ofisi yao na kutojulikana walipokuwa na baada ya kutafutwa na waandishi wa habari kujua kulikoni hawaonekani wakati wametangaza kuandamana,mwenyekiti wa chama hicho mkoa Peter Machanga alidai kuwa leo walikuwa wanawaandaa tu wananchi kwa ajili ya maandamano yatakayotangazwa rasmi.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Shinyanga mjini walisema huenda maandamano hayo yamesitishwa kutokana na askari wa jeshi la polisi kutapakaa mitaani kwa ajili ya kukabiliana na yeyote mwenye kujitokeza kuandamana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo