Msanii wa muziki Florah Mbasha, Baada ya kufunguka mengi kuhusiana na matatizo katika ndoa yake wiki hii, ameweka wazi kuwa shughuli zake za muziki bado zinaendelea huku akiwa na albam mpya kabisa kwaajili ya wapenzi wa sanaa yake.
FLorah
Mbasha amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya
inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda, kazi ambayo tayari jamii
imeipokea vizuri.
Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi hii.
Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi hii.