WALIOKUFA BAADA YA BOMU KUTUPWA KWENYE GARI HUKO KIGOMA WAFIKIA WANNE

MAJERUHI Regina Mzakule (66) amefariki dunia na kufanya idadi ya waliokufa katika tukio la bomu la kutupa kwa mkono ndani ya gari la abiria wilayani Buhigwe, Kigoma kufikia wanne.

Bomu hilo lilitupwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi.

Akizungumza nasi, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Joshua Monge alisema alipokea majeruhi saba wa tukio hilo akiwemo marehemu huyo.

Alisema mrehemu huyo alipata majeraha makubwa na vipande vya chuma kumuingia tumboni.

Aliwataja majeruhi watatu walioruhusiwa kuwa ni Honolina Benjamini (42), Kabula Matius (40) na Agripina Jeremia (45) wakati wanaoendelea na matibabu ni Shukrani David (32), Tedy Charles (25) na Osward Samweli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo